Anthony Martial anakaribia kusaini AEK Athens kwa uhamisho wa bure, huku klabu hiyo ikiandika kwenye akaunti yao ya Twitter kwamba atawasili uwanja wa ndege saa 20.40 usiku wa leo.
Martial aliondoka Manchester United majira ya joto mkataba wake ulipoisha na amekuwa akihangaika kutafuta klabu mpya.
Gazeti la Ugiriki la Fos linasema kwamba kijana mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kuvunja masharti ya mkataba wa miaka mitatu.
Martial atajiunga na winga mwingine wa zamani wa Ligi Kuu katika AEK, huku nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur Erik Lamela akisajiliwa mnamo Julai.