Mwanamume huko Brazil aliye kuwa na shoka dogo alipanda ukuta ndani ya chumba cha kulelea watoto Kusini mwa Brazili na kuwaua watoto wanne siku ya Jumatano, na kuwajeruhi wengine watano katika shambulio hilo.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 25 alijisalimisha kwa polisi baada ya ghasia hizo, mkuu wa polisi Marcio Alberto Filippi aliwaambia waandishi wa habari.
Polisi walisema wavulana watatu wawili wa miaka 4 na mmoja wa miaka 5 na msichana mmoja wa miaka 7 waliuawa.
Watoto wanne kati ya waliojeruhiwa wenye umri wa kati ya miaka 3 hadi 5 walikuwa wakitibiwa hospitalini na waliripotiwa kuwa katika hali nzuri, huku mtoto wa tano akiwa na majeraha madogo, polisi walisema.
Mshambuliaji huyo alikuwa na historia ya vurugu na dawa za kulevya, na aliwahi kumchoma kisu baba yake mlezi mnamo Machi 2021, polisi walisema.
Kutokana na tukio hilo Rais wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva alisema katika chapisho la Twitter kulingana na jarida la Reuters kuwa;
“Janga kama hili halikubaliki, kitendo cha kipuuzi cha chuki na woga na ni kitendo cha unyanyasaji dhidi ya watoto wasio na hatia na wasio na ulinzi,”