Mwanafunzi mmoja nchini India anayejiandaa kwa mitihani ya bodi ya shule ya sekondari alilazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kwa sababu ya kuganda kwa damu iliyosababishwa na matumizi ya dawa za ‘kuzuia usingizi’ kupita kiasi.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, kituo cha Lucknow mwanafuzi huyo alikuwa akitumia dawa hizo kwa muda mrefu, na kusababisha uvimbe wa neva na kusababisha kulazwa hospitalini.
Kulingana na ripoti ya ANI, wakati wa mitihani ya bodi ya CBSE inayoendelea, wanafunzi wengi wanageukia dawa za kuzuia usingizi ili kuchelewa kulala na kusoma, na kuvuruga mizunguko yao ya kulala.
Wanafunzi hawa pia wanaongeza ulaji wao wa kafeini kupitia chai au kahawa ili kutopata usingizi mtindo huu mbaya wa maisha unaathiri vibaya afya zao, na hivyo kuzua maswali kuhusu uhalali wa dawa hizi.