Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 35 kutoka Jimbo la Chhattisgarh, India, amefariki dunia baada ya kumeza Kifaranga cha kuku kilicho hai katika kitendo kinachodhaniwa kufanywa kama sehemu ya tiba ya kishirikina ya matatizo ya uzazi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Madaktari walioufanyia mwili uchunguzi walibaini kifaranga hicho cha urefu wa sentimita 20 kikiwa hai nakuziba njia ya hewa na chakula hali iliyosababisha Marehemu Anand Yadav kufariki kwa kukosa hewa huku Daktari Santu Bag, aliyefanya uchunguzi huo alisema kuwa hajawahi kukutana na tukio la aina hii katika taaluma yake ya uchunguzi wa miili zaidi ya 15,000.
Inadaiwa kuwa Anand, aliyekuwa akihangaika na matatizo ya uzazi alikwenda kwa Mganga wa kienyeji ambaye huenda alimshauri kufanya kitendo hicho kwa imani kuwa ingesaidia kupata Mtoto.
Aidha Polisi wameanza uchunguzi kubaini mazingira ya tukio hilo na mchango wa imani za kishirikina ambapi tukio hili limeibua mjadala mpana kuhusu madhara ya imani potofu na haja ya elimu sahihi kuhusu afya.