Promise Ibeh (15), binti anayetoka eneo la serikali ya mtaa ya Umunneochi katika jimbo la Arabia nchini Nigeria ambaye alipata alama za juu za A9 katika mtihani wake wa cheti cha shule ya upili ya Afrika Magharibi WASSCE, ameuawa na mama yake wa kambo baada ya kupata ufadhili wa kimasomo nje ya nchi.
Msichana huyo, baada ya kufaulu alipata ufadhili wa kutafuta masomo ya uhandisi wa Programu nchini Uingereza, ambapo inadaiwa kitendo hicho hakikumfurahisha mama huyo aliyeshikwa na wivu wa kupindukia, hali iliyopelekea kukatisha uhai wake kwa kumpa chakula chenye sumu.
Mmoja wa watu walioshiriki maziko ya binti huyo, Ofoke Bright Ikenna alisema mkono wa uovu uliomkumba Promise haukuwa mwingine ila wa mama yake wa kambo, aliyetumia mchanganyiko wa sumu wa wivu na kinyongo cha binti wa mumewe kupata ufaulu mkuu na ufadhili wa masomo, ni ajabu kabisa.
Tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mama huyo kwa uchunguzi Zaidi, na taarifa za tukio hilo zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kabla na baada ya mazishi hali iliyopelekea watu kumshambulia mama huyo kwa maneno huku baadhi ya ndoa zikitetereka hasa zile zenye familia ya mchanganyiko wa Watoto wenye wazazi tofauti wanaoishi Pamoja.