Mwanamume mwenye umri wa miaka 32 amekamatwa kwa madai ya kumtukana Rais wa Kenya William Ruto na kupambana na maafisa wa polisi katika uwanja wa Jacaranda eneo la Eastlands Nairobi kumkamata.
Shandrack Omondi Orwa alishtakiwa kwa kusababisha fujo kwa namna ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani kinyume na Kifungu cha 95 (1) (b).
Bw Omondi alishtakiwa kwa kupiga kelele na kutamka maneno “Maandamano tutaenda,makarao ni wachache wataumia serious ,tutaonesha kuna maafisa wachache wa polisi wataumia” kwa
maafisa wa polisi waliokuwa doria katika eneo hilo.
Mshukiwa huyo kwa kushirikiana na wenzake wanadaiwa kuwachochea wananchi kufanya vurugu dhidi ya askari polisi waliokuwa wakishika doria katika viwanja hivyo kwa kutishia kuwapiga mawe.
Wakati wa uchunguzi, Bw Omondi aliambia DCI kwamba anajutia maneno aliyotumia dhidi ya rais na polisi.
Aliachiliwa kwa bondi ya Sh50,000 na dhamana mbadala ya pesa taslimu Sh20,000.
Kesi hiyo itatajwa Juni 5 kabla ya kuanza kusikilizwa Julai 17 mwaka huu.