Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, leo Auguts 24 Mkoani Morogoro amempongeza Afisa Ugani Wilaya ya Kibaha, Joseph Njau baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nikson John (Nik wa Pili) kumueleza upambanaji wa Afisa Ugani huyo ambaye hutembelea kila nyumba za Wakulima na kuwafundisha kilimo.
Afisa Ugani huyo amepongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi ya kusimamia shughuli za kilimo Wilayani Kibaha ambapo pongezi hizo zimekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, DC Nickson kumwelezea Katibu Mkuu juu ya utendaji kazi mzuri wa Afisa huyo ambaye hutembelea kila nyumba za wakulima na kuwafundisha kilimo.
Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo wakati wa ufunguaji wa mafunzo ya matumizi na usimamizi bora wa vifaa vya kisasa vya kilimo kwa maafisa ugani wa 132 wa Kanda ya Mashariki na Kusini.