Huku kukiwa na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas, kundi la wanamgambo wa Palestina lilisema kuwa linakadiria kupoteza wapiganaji wake wapatao 6,000, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Afisa wa Hamas aliyeko Qatar aliiambia Reuters kwamba licha ya hayo, kundi hilo linaweza kuendelea na mapigano na liko tayari kwa mzozo wa muda mrefu huko Rafah na Gaza.
“Chaguo za Netanyahu ni gumu na kwetu pia. Anaweza kuikalia Gaza lakini Hamas bado imesimama na kupigana. Hajafikia malengo yake ya kuua uongozi wa Hamas au kuwaangamiza Hamas,” aliongeza.
Idadi iliyoelezwa na Hamas ni takriban nusu kama ilivyoripotiwa na jeshi la Israel, ambalo linasema wapiganaji 12,000 kutoka kundi tawala la Gaza wameuawa katika mzozo huo.
Matamshi ya kundi hilo la wapiganaji ni nadra kukiri kwamba limevumilia hasara kubwa katika mapigano ya Gaza.