Polisi nchini Uhispania imemkamata mmoja wa maafisa wake wakuu wa polisi baada Bill 56,492,000,000 na cocaine kupatikana kwenye kuta za nyumba yake.
Uchunguzi kuhusu kisa hiki kikubwa nchini humo ulifanyika ghafla nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na utakatishaji fedha na kupatikana kwa madawa ya kulevya pamoja na pesa taslimu
Maafisa walimkamata wiki iliyopita pamoja na watu wengine 15, akiwemo mpenzi wake , ambaye pia ni afisa wa polisi katika mkoa wa Madrid, chanzo cha polisi kilisema bila kumtaja.
Wakati wa uvamizi huo, polisi walipata euro milioni 20, pesa taslimu, zikiwa zimefichwa kwenye kuta na dari za nyumba ya wanandoa hao huko Alcalá de Henares, mji wenye wakazi wapatao 195,000 ulio umbali wa maili 18 (30km) mashariki mwa mji mkuu wa Uhispania.
Óscar Sánchez Gil hadi hivi majuzi bado alikuwa mkuu wa kitengo cha udanganyifu na kupinga utakatishaji fedha cha jeshi la polisi la kitaifa la Uhispania huko Madrid.