Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema Afrika inahitaji ujuzi na uwezo wa kutengeneza chanjo yake. Kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika, amesema ulimwengu ulikuwa ukishuhudia “Chanjo ya ubaguzi wa rangi”.
Na ni ukweli kwamba kati ya mamia ya mamilioni ya chanjo ambazo hadi sasa zimetolewa, chini ya asiliamia 2 zimewafikia Waafrika. Mpaka sasa Afrika ina idadi ndogo ya maambukizi ya Covid-19 ikilinganishwa na Ulaya na Marekani.
Hii ni kwasababu serikali nyingi za Afrika zilichukua hatua haraka ya kufunga mipaka na kuweka vizuizi.
Shirika la Afya duniani(WHO) limetahadharisha kuwa wimbi jingine la maambukizi huenda likarejea na kuwa nchi zilizo na mifumo duni ya afya zinaweza kuathirika.