Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza mshikamano wake na Wapalestina mbele ya jinai za kutisha zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina hao wasio na ulinzi.
Akiwa amevaa skafu ya Palestina, Rais Ramaphosa amesema: “Njia kuu ya kushughulikia mgogoro wa Palestina ni kuheshimishwa sheria na maazimio ya kimataifa likiwemo suala la kutangaazwa nchi huru ya Palestina.
Aidha amesema: “Tunatuma rambirambi zetu kwa familia za wahanga wa kiraia wakati wa mapigano ya hivi karibuni kati ya pande mbili.” Vilevile amelaani njamaa za utawala wa Kizayuni za kutaka kuwahamisha Wapalestina akisema: “Amri ya Israel ya kuwahamisha zaidi ya watu milioni moja kutoka kaskazini mwa Ghaza hadi kusini itafanya mambo kuwa mabaya zaidi.”
Amesisitiza kwa kusema, Afrika Kusini itaendelea kushikamana na watu wa Palestina na itaendelea kuunga mkono suluhisho la amani.”
Ameongeza kuwa, iwapo amani itapatikana huko Palestina, amani hiyo italifaidisha eneo zima la Asia Magharibi. Ukanda wa Ghaza, ambao umezingirwa na Wazayuni makatili tangu mwaka 2006, umeshambuliwa akikatili na Israel na kuharibiwa vitongoji vyote.
Mamia ya maelfu ya wananchi wa kawaida wa Palestina wameshauawa shahidi, kujeruhiwa na kuwa wakimbizi tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha jinai zake hizo Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba, 2023.