Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kuzingatia iwapo mpango wa Israel wa kuendeleza mashambulizi yake huko Gaza hadi katika mji wa Rafah unahitaji hatua za ziada za dharura kulinda haki za Wapalestina.
Katika taarifa, siku ya Jumanne, ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema kuwa imewasilisha “ombi la dharura” kwa ICJ siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa serikali “ilikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba mashambulizi ya kijeshi ambayo hayajawahi kutokea dhidi ya Rafah, kama ilivyotangazwa na Taifa la Israel,”
alisema tayari imesababisha na itasababisha mauaji makubwa zaidi, madhara na uharibifu.
Mwezi uliopita, Mahakama ya Dunia iliiamuru Israel kuchukua hatua zote kuzuia wanajeshi wake kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini.