Klabu ya Azam FC ambayo inajiandaa kusafiri kwenda Zambia kuweka kambi ili kujiandaa na michuano ya kimataifa, January 25 ilishuka dimbani katika uwanja wa Karume kucheza mechi yake ya Kombe la FA dhidi ya klabu ya African Lyon.
Azam FC ambao wanahasira ya kutolewa Mapinduzi Cup kwa mara ya kwanza katika hatua ya Makundi, huku wakiweka rekodi ya kutolewa bila kushinda mchezo wowote, wamefanikiwa kuifunga African Lyon kwa jumla ya goli 4-0.
Timu hiyo inayofundishwa na Stewart Hall imefanikiwa ilianza kupata goli la kwanza dakika ya 1 kupitia kwa kiungo wake Mudathir Yahaya, wakati goli la pili na la tatu yalifungwa na Farid Mussa dakika ya 3 na 37, Ame Ally alipachika goli la nne na la mwisho dakika ya 54 ya mchezo. Kwa sasa Kombe la FA litaingia hatua ya 16 bora.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.