Baada ya serikali kufungia TV kwa siku 7 Leo February 6, 2018 nakusogezea stori ambayo inashika headline Nchini Kenya ambapo imekuwa ni Good News kwa watazamaji wa televisheni ya KTN na NTV ambapo matangazo ya vituo hivyo viwili yamerejea hewani.
Lakini bado Wakenya ambao hawana king’amuzi hawawezi kutazama. Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving’amuzi vya “Dstv, GoTV and Zuku.
Stesheni hiyo ilikuwa ni mojawapo TV zilizoathirika na hatua ya serikali kufungia vituo vya TV baada ya kuonesha kuapishwa kwa Raila Odinga, Citizen TV bado haijafunguliwa.
MKAPA, JK, LOWASSA, MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WALIVYOUAGA MWILI WA KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA