Mwanamama wa Ghana Afua Asantewaa Aduonum yuko katika safari ya kuvunja rekodi ya dunia ya kuwa mshindi wa mbio ndefu zaidi za kuimba.
Katika jaribio lake la kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness na Sunil Waghmare, Mhindi ambaye aliimba kwa saa 105 mwezi Machi 2012, Afua nae amekuwa akiimba nyimbo za Ghana mfululizo katika kijiji cha Akwaaba.
Safari ya Afua iliyoanza usiku wa manane mnamo Desemba 24 inatarajiwa kumalizika Desemba 27, ambayo inamaanisha kuwa atakuwa akiimba bila kukoma kwa siku 4 na masaa 9.
Mama huyo wa watoto 2 amekuwa akiimba nyimbo za Ghana mwanzo hadi mwisho katika kijiji cha Akwaaba ambapo idadi ya Waghana wakiwemo wanamuziki wa maarufu na wanasiasa wamekusanyika ili kumuunga mkono.
Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia pia alikuwepo kuunga mkono jitihada za mama huyo.