Mwanamke wa California alihukumiwa siku ya Jumatatu kifungo cha zaidi ya miaka mitatu jela katika kesi ya muda mrefu kwa kilichosemekana kuwa biashara yakusaidia wanawake wajawazito wa China kusafiri hadi Marekani kujifungua watoto ambao walikuja kuwa raia wa Marekani moja kwa moja.
Waendesha mashtaka wa shirikisho walidai kuwa Dong na mume wake waliotengana sasa Michael Liu walisaidia zaidi ya wanawake 100 wajawazito wa China kusafiri hadi Marekani.
R Gary Klausner, hakimu wa wilaya wa Marekani, alimpa Phoebe Dong kifungo cha miezi 41.
Dong na mumewe walihukumiwa mwezi Septemba kwa kula njama na utakatishaji fedha kupitia kampuni yao, USA Happy Baby.
Wakati wa kusikilizwa kwa hukumu katika mahakama ya shirikisho huko Los Angeles, Dong alifuta machozi alipokumbuka alikua bila ndugu kutokana na sera kali ya China ya “mtoto mmoja”.
Aliiambia mahakama ya shirikisho huko Los Angeles kwamba serikali ya China ilimlazimisha mama yake kutoa mimba.
Mamlaka zilisema kuwa wawili hao waliwafundisha wanawake jinsi ya kuwalaghai maafisa wa forodha kwa kuruka katika viwanja vya ndege vinavyoaminika kuwa na ulegevu wa usalama zaidi huku wakiwa wamevalia mavazi yanayoficha mimba zao.