‘Wanawake wengi hawataki kwenda hospitali kupata huduma zinazohusiana na afya ya uzazi na hivyo kuilazimisha serikali kuanza kutoa gari maalum litakalowafuata kwenye makazi yao,’ Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijibu swali bungeni.
Alikuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula aliyetaka mkakati wa serikali kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinaisha kabisa kwenye jimbo lake.
Akjibu, waziri Ummy alisema kuwa ukiona wanaume wanazungumzia masuala ya uzazi wa mpango basi sasa mambo siyo mabaya.
Amesema kuwa wanawake wengi hasa wa mijini hawapendi kwenda na kukaa kwenye huduma za afya kwa masaa mengi.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo alisema kuwa serikali sasa imekuja na mpango wa huduma za uzazi wa mpango zinazotembea.