Kila tarehe 24 March dunia huadhimisha siku ya ugonjwa wa kifua kikuu, Siku hii ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.
Leo March 24 2016 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alikutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuelezea kuhusu changamoto za ugonjwa huo.
‘Kifua kikuu ni ugonjwa unaoambukizwa na bakteria wanaojulikana kwa jina la Mycobacteria tuberculosis, vimelea vyake huenea kwa njia ya hewa na havichagui aina ya mtu pia hutoka kwa mgonjwa ambaye hajaanza matibabu na kuambukiza wengine‘ ;-Ummy Mwalimu
‘Licha ya kuwa kifua kikuu kinatibika, lakini ndio ugonjwa pekee wa kuambukiza unaosababisha vifo vya watu wengi katika jamii, ambapo watu watatu hufariki kila baada ya dakika moja. Takwimu zinaonyesha Tanzania takribani watu 12,000 hufariki kwa ugonjwa huu‘ ;-Ummy Mwalimu
‘Natoa wito kwa wananchi wote kuwa na kawaida ya kufanya uchunguzi wa afya zao ili kugundua tatizo mapema na kuzuia kuenea kwa Kifua kikuu, tukifanya hivyo tutapunguza kuenea kwa ugonjwa huu‘ ;-Ummy Mwalimu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE
Ilikupita hii Video ya Sentensi za Waziri wa Afya kuhusu wazee na usumbufu hospitalini?