Leo February 3, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 197 kuwa Luteni Usu kati ya hao wanawake wakiwa ni 28 katika shughuli iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Sherehe hizo maafisa hao wapya wa Jeshi, viongozi mbalimbali wa serikali, akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ulinzi na Usalama, Dr. Hussein Mwinyi nao walihudhuria.
Wengini ni Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, General Venance Mabeyo, wakuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama wastaafu pamoja na viongozi wa majeshi ya nchi jirani ambao baadhi ya wanajeshi wao wametunukiwa leo wakiwemo kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi pamoja nchi nyingine rafiki.
Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao, Rais Magufuli alikagua gwaride na baadaye kutoa zawadi kwa maafisa wanne waliofanya vizuri katika mafunzo.
Waliotunukiwa ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki ambao walipata mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha
MAZISHI JUMATATU: BADO HAIJULIKANI NI DINI GANI ITAMZIKA MZEE KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA