Beki wa Azam FC Agrey Morris baada ya kutangazwa kuwa January 12 2021 ndio atastaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa kwa kuagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Congo DR uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
AyoTV akiwa visiwani Zanzibar walitaka kufahamu Morris baada ya kutangaza kustaafu timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 36 kwa ngazi ya club atacheza hadi lini?
“Huu ni muda sahihi wa mimi kustaafu kama mimi niliachiwa kijiti na Kusi na mimi umefika muda wa kuachia vijana nafasi, umri wangu sasa hivi umesogea na vijana wanakuja kwa kasi ukiangalia kuna Sebo, Ame na Mwamnyeto kwa hiyo huu ni muda wangu sahihi kwa Azam FC nitastaafu 2022 nikimaliza mkataba wangu huu wa miaka miwili”>>> Agrey Morris
Morris ameeleza hayo na kusema kuwa amejitathmini na kuona huu ni muda sahihi kwake hakutaka acheze akiwa na heshima yake hadi kiwango kishuke watu waanze kumzomea.