Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kununua kila goli litalofungwa na Club za Simba na Yanga katika michuano ya kimataifa kwa shilingi milioni tano ileile, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameeleza.
Gerson Msigwa akihojiwa na LEO TENA ya Clouds FM amesema kila goli litakalofungwa na Timu hizo katika mashindano ya Kimataifa litanunuliwa na Rais Samia kwa pesa ileile ya Tsh. milioni 5 wakati huu ambao Yanga inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Shirikisho huku Simba ikiiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Club Bingwa Afrika.
Jumapili iliyopita Rais Samia alitimiza ahadi hiyo kwa kutoa shilingi milioni 15 kwa Club ya Yanga baada ya Timu hiyo kuifunga TP MAZEMBE ya Congo magoli matatu kwa moja (3-1).