Mwanaume mmoja kutoka Kijiji cha Gichugu Kaunti ya Kiriyanga nchini Kenya ameharibu mazao yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi za Kenya 200,000 (sawa na Milioni 4.3 ) baada ya mke wake kukataa kubaki nyumbani kusherekea Siku ya Kina Baba Duniani.
Kwa mujibu wa mashahidi, mwanaume huyo alitumia panga kuharibu furushi la ndizi na maparachichi za mkewe pamoja na wafanyabiashara wengine waliokuwa wakijiandaa kwenda kuziuza sokoni siku ya Jumapili baada ya mwanamke huyo kusisitiza kwenda kuuza sokoni siku ya Jumapili.
Mwanaume huyo alitaka mkewe abaki nyumbani kwa kuwa ilikuwa siku ya akiba baba duniani. Mkewe hujipatia riziki yake kwa kuuza matunda katika soko la Kitui siku ya Jumapili
“Mimi ni mmoja wa wale vitu zao zimeharibiwa, tumefanya uchunguzi tukajua kwamba aliyeharibu ni bwana ya mama mmoja tunaenda na yeye soko,” Hellen Kaari Muriithi, mmoja wa wafanyabiashara walioharibiwa mali zao aliuambia Mtandao wa Citizen, akisema alipewa taarifa ya bidhaa zake kuharibiwa na madereva bodaboda.
Tukio hilo limewaacha wakazi wa eneo hilo vinywa wazi, huku wafanyabiashara wasijue hatua gani hasa ya kuchukua dhidi ya mwanaume huyo, na ikiwa watalipwa fidia.