Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amesomewa shtaka moja la kumtukana Rais John Magufuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mdee alisomewa kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa na wakili wa serikali Nassoro Katuga ambapo imeelezwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
#BREAKING Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili, ushahidi haujakamilika kesi imeahirishwa hadi August 7, 2017. pic.twitter.com/C43WqfTO40
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Katuga alidai kuwa July 3, 2017 katika Ofisi za Chadema makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia ” Anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afunge break,”. Baada ya kusomewa kosa hilo, Mdee alikana kosa.Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika anaomba kesi iahirishwe.
Mdee amedhaminiwa kwa bondi ya shilingi milioni kumi na wadhamini wawili ambapo kesi imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.
VIDEO: Umepitwa na hii ya William Ngeleja kurejesha fedha za mgao wa ESCROW? Bonyeza play hapa chini.