Mabingwa wa Ligi Kuu England klabu ya Leicester City, leo July 8 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria aliyekuwa anaichezea klabu ya CSKA Moscow ya Urusi Ahmed Musa, Leicester wamemsajili Musa kwa mkataba wa miaka minne.
Musa ambaye ana umri wa miaka 23 amesajiliwa kwa ada ya uhamisho wa rekodi unaokadiriwa kufikia pound milioni 18, staa huyo wa Nigeria anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Leicester City, baada ya kusajiliwa Nampalys Mendy, Ron-Robert Zieler na Luis Hernandez. Musa amefunga jumla ya goli 54 katika mechi 168 akiwa CSKA.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mbwana Samatta aliwahi kukiri kuwa na urafiki na Ahmed Musa, baada ya mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria uliochezwa September 5 2015 uwanja wa taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu ya 0-0.
Congratulations to Ahmed Musa on his move to English Champions Leicester City. Paint the EPL green with goals. pic.twitter.com/y655tKCp2i
— Nigeria Super Eagles (@NGSuperEagles) July 8, 2016
Baada ya mchezo walibadilishana jezi na Samatta kusema Musa alimsaidia alipokuwa katika majaribio CSKA Moscow kutokana na yeye kutokujua lugha ya kirusi, hivyo Musa ndio alikuwa mtu wake wa karibu kutokana na kuwa na uwezo wa kuwasiliana nae kwa lugha ya kiingereza.
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1