Ni Agosti 15, 2023 ambapo kikosi cha Simba SC kimeanza mazoezi rasmi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Agosti 17, 2023 mwaka huu katika Uwanja wa Manungu Turiani.
Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema timu hiyo inaendelea vizuri na mazoezi hadi sasa wachezaji wawili ndio wataukosa mchezo huo wa Mtibwa ambao Aishi Manula na Inonga ambaye aliumia wakati wa mchezo nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Foutain Gate.