Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uzalishaji na uuzaji wa Maziwa ‘Asas’, Ahmed Asas ambae leo June 6, 2023 ameeleza kile kilichoandaliwa katika kuelekea kampuni ya Uhamasishaji kutoa Elimu juu ya Maziwa visiwani Zanzibar.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV alisema..’Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa watanzania kwa kutuwezesha Asas Daires kuwa namba moja katika mashindano ya maziwa kati ya makampuni yote Tanzania ambapo wiki iiliyopita kwenye maadhimisho ya wiki ya Maziwa kule Tabora tunapata faraja sana ya kuendelea kujituma na kuongeza ubunifu kila siku’- Ahmed Asas
‘Lingine la msingi ni kuhusiana na Kampeni ya Uhamasishaji tuliyoipa jina la Jali Afya na Asas ambapo kwa ndugu zetu kule visiwani Zanzibar wameshaanza tangu June 4, 2023 na kampeni hii ya uhamasishaji kuhusu Maziwa ambapo itahusisha maeneo yafuatayo yakiwemo Mashuleni, Vikundi vya Wanawake na Wajasiriamali, Wapishi, Maduka ya Jumla na Reja Reja, Vikundi vya Mazoezi’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas, Bw Ahmed Asas
‘Na Mnamo June 17, 2023 hitimisho la kampeni yetu itafanya Katika Viwanja vya Kisonge kuanzia saa kumi na mbili alfajiri ambapo kutakuwa na mambo yafuatayo yakiwemo Mazoezi ya kukimbia, Maonesho ya bidhaa za Maziwa, Burudani na Michezo pamoja na Elimu juu ya unywaji wa maziwa’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas, Bw Ahmed Asas
‘Bila kusahau tutakuwa na mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, sisi kama Asas tunaomba wadau na wananchi wote waendelee kukaa na platform zetu tutakuwa tunaendelea kuwahabarisha kwa kile kilichosahihi hakika maziwa ni Afya’- Ahmed Asas