Ikiwa Agosti 8, 2023 yamefanyika kilele cha maandhimisho ya Sikukuu ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika vieanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya sasa leo Kampuni ya Uuzaji wa Maziwa nchini Asas Dairies Ltd na Afrifam kupitia Mkurugenzi wake aitwae Ahmed Asas ametunukiwa vyeti viwili.
Ahmed amepewa cheti cha Ushindi kupitia Asas Dairies Ltd ikiwa kama wanaongoza kitaifa kundi la wasindikaji/wachakataji wa Mazao (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na cheti cha pili cha Ushindi katika kundi la Wakala wa kwanza wa pembejeo.
Aidha Ahmed Asas akizungumza na millardayo.com alisema..’Kiukweli hii ni kubwa sana ningependa kuwashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini sisi kama Asas tunawaamini kutoacha kuwahudumia suala la maziwa na nikukumbushe tu unywaji wa maziwa ni Afya tele hivyo hakikisha hata kwa siku kunywa glasi moja ya Asas ili uujenge mwili na kuendelea kulitumikia Taifa letu linaloongozwa na Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan’
‘Jana tulipata ugeni wa Rais wetu mengi tumezungumza nae tumemuonesha bidhaa zetu hayo yote ni kupitia Nanenane hivyo sisi kama Asas na Afrifam ni hatua kubwa na Elimu hii itaendelea sio mwisho kwenye Nanenane basi itakuwa na mwendelezo wake’- Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa Maziwa Ahmed Asas