Ditrick Muogofi (43) amehukumiwa kunyogwa hadi kufa kutokana na kosa la mauaji aliyoyatekeleza katika Kijiji cha Itulike Kata ya Ramadhani Mjini Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamod Hassan Banga ametoa taarifa kuhusu hukumu hiyo ya kesi ya mauaji No 53 ya mwaka 2023, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya oparasheni mbalimbali za Polisi Njombe kwa kipindi cha kuanzia September 1 mpaka October 31,2023 ambapo pia amesema katika kipindi hicho Alex Simon Gwavi (65) alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka Mtoto wake wa kike huko Mundindi katika Wilaya ya Ludewa.
“Ditrick Muogofi huyu alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji huko katika Kijiji cha Itulike, Ramadhani Njombe lakini kuna Mtu anaitwa Alex Simon alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka Binti yake katika Kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa kwa kesi namba 44 ya mwaka 2023”