Mchina mmoja aliyetambulika kwa jina la ukoo tu la Gu, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kutuhumiwa kuwatisha kuku 1,100 wa jirani yake hadi kufa, katika mpango wa kulipiza kisasi.
Kulingana na gazeti la ‘China Daily,’ Gu alivuka mipaka mara mbili na katika tukio la pili, alitumia tochi kuwatia hofu ndege wa jirani yake ambpo hatimaye ilisababisha machafuko makubwa kati ya ndege hata kuanza kushambuliana..
Inavyoonekana, mara ya kwanza Gu alipoamua kuingia kwa siri ndani ya uwa wa jirani yake, kuku 500 walikufa baada ya kukanyagana hadi kufa. Maafisa wa polisi wa eneo hilo hatimaye walimkamata Gu na kumwamuru amlipe jirani yake, aliyetambuliwa tu kama Zhong, yuan 3,000 (kama $436 USD) hata hivyo, hii ilimkasirisha zaidi Gu na kumfanya aingiwe na wasiwasi mwingine.
Kwa hivyo, alirudi kwenye ua wa Zhong mara ya pili na kuua mamia ya kuku zaidi kwa tukio la tochi. Mamlaka zinasema kuwa jumla ya kuku 1,100 waliuawa kati ya mauaji hayo mawili.
Pia inaelezwa kuwa matukio hayo mawili yalikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa kulipiza kisasi, kutokana na ugomvi unaoendelea kati ya majirani hao wawili.
Inaripotiwa kwamba mambo yote yalianza mnamo Aprili 2022 wakati Gu alipokata baadhi ya miti ya Zhong bila idhini yake.
Mahakama ya Hengyang hatimaye iliamua kwamba Gu “alisababisha hasara ya mali kwa makusudi” kwa Zhong, na kumwacha na hasara ya yuan 13,840 (yaani $2,015 USD).
Tangu matukio haya yote Gu amehukumiwa kifungo cha miezi sita, na mara tu atakapoachiliwa, basi atalazimika kutumikia mwaka mzima kwa majaribio ya kubadilisha tabia.