Jioni ya May 27 2016 kulitokea ajali ya Mtumbwi uliozama Bahari ya Hindi, watu waliokuwa kwenye mtumbwi huo walikuwa wakivuka kutoka soko kuu Feri kuelekea Kigamboni Dar es salaam. Mtumbwi huo unasadikika kubeba watu zaidi ya 16 ambao baadhi yao wametoka wazima.
Siku ya jana Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kuwapata watu nane ambapo mmoja wao alipoteza maisha. kutokana na changamoto ya giza shughuli ya uokoaji iliahirishwa na ikaendelea leo May 28 2016 ambapo miili mingine ilipatikana na kufikia jumla ya miiili ya watu watano.
Chini kwenye video hii fupi ni Mratibu msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bashir Mazehebi akieleza zoezi la uokoaji lilivyokuwa
ULIIKOSA TAARIFA YA GARI LILILOZAMA DAR ES SALAAM APRIL 20 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUB