Watu wawili waliuawa na wanne kujeruhiwa wakati moto ulipoteketeza jengo la makazi mjini Johannesburg mapema Jumapili, maafisa wa jiji hilo walisema, na kuongeza shughuli za utafutaji na uokoaji bado zinaendelea.
“Operesheni ya moto inaendelea katika jengo la ghorofa mbili ambalo liliteketea kwa moto mapema leo asubuhi,” Idara ya Huduma za Dharura ya Jiji la Johannesburg ilisema katika taarifa.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini tarehe 21 Januari viliripoti kuwa ajali ya moto imetokea kwenye jengo moja la ghorofa lililoko kwenye eneo kuu la biashara mjini Johannesburg, hadi sasa watu wawili wamethibitishwa kufariki na wengine wengi wamejeruhiwa, na watu takriban 150 wamepoteza makazi yao.
Meya wa Johannesburg Kabelo Gwamanda amesema hatua mbalimbali zinachukuliwa mara moja ili kutatua tatizo la makazi kwa walioathirika katika ajali hiyo.