Leo May 30, 2018 nakusogezea stori kutoka nchini Kenya ambapo Benjamin Gsel mwenye miaka 26 aliyezaliwa Vienna nchini Austria ameacha kazi Dubai na kwenda kuuza mitumba Nairobi nchini .
Kwa mujibu wa Benjamin anasema kuwa kwa mara ya kwanza alifika Kenya mwaka 2007 na alivutiwa na wafanyabiashara wa mitumba jinsi walivyokuwa wakifanya biashara hiyo na akaamua kufanya utafiti mdogo juu ya biashara ya mitumba na mwaka uliopita mwezi September aliamua kuacha kazi yake huko Dubai na kuja Kenya kufungua biashara ya Mitumba.
Benjamin ambaye kwa miaka saba amekuwa akifanya kazi za mashirika (Corporate World) mjini Dubai kwa sasa ana maduka matatu ya mitumba Nairobi yanayouza mitumba jumla jumla na anasema kwamba alianza kwa mtaji wa shilingi 5500,000 za Kenya ambayo ni sawa na shilingi 132,000,000 za kitanzania ambazo zilitokana na akiba aliyokuwa amejiwekea na mchango mwingine kutoka kwa mshirika wake.
Aidha Benjamin anasema kuwa mitumba yake anaitoa Uingereza na aliamua kufanya kazi nchini Kenya kwa sababu anaamini kuwa nchi hiyo ndio inaongoza kwa soko la mitumba katika Afrika Mashariki lakini pia lugha ya kiingereza sio tatizo hivyo inakuwa rahisi kufanya biashara nchini humo pamoja na kuwa na hali tulivu ya kisiasa.