Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kumshikilia kwa Mahojiano Yassir Seif Mkaazi wa Tomondo Zanzibar kwa kuamua Kujiteka yeye mwenyewe baada ya kuhitaji kiasi cha Fedha ili afungue Biashara ya kutuma na kutoa fedha
Yassir amesema alijiteka kwa siku tatu na alikua akilala kwenye nyumba za Ibada (Msikitini) huku akiidanganya familia yake kua ametekwa na kwamba mtekaji anahitaji kiasi cha shillingi Laki Sita ili amuachie kijana huyo aliejitaka
Baada ya Jeshi la Polisi kumsaka na kufanikiwa kumshikilia yassir alimueleza Kamanda wa Polisi ACP Richard Mchomvu kua alitumiwa shillingi Laki Mbili na Familia Licha ya kuhitaji Laki Sita lakini aliamua Kucheza Mchezo wa Kubeti na Hadi kufanikiwa kufikisha Laki sita ili afungue biashara hiyo ya Kutuma Pesa na kutoa pesa