Taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita inahusu ajali ya kuanguka kwa Jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa.
Mtu mmoja amefariki na wafanyakazi na wakazi wengine wa eneo la Ruaraka, Kenya wamenusurika kifo kutokana na ajali ya kuanguka kwa jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa, kwa mujibu wa mashuhuda wanasema ajali hiyo imesababishwa na nyufa zilizokuwa katika jengo hilo.
Taarifa ya Citizen News imesema wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba waliwahi kuwakemea wamiliki wa jengo hilo kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango lakini hakuna mabadiliko yaliyowahi kufanyika.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu iliyopelekea ajali hiyo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook