Msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ndio huu, Chrismas imemalizika na tunasubiri mwaka mpya, wakati tukisubiri mwaka mpya millardayo.com na Ayo TV imempata kwenye exclusive interview kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Mohammed Mpinga ambapo amezungumzia takwimu za madaereva walevi Dar es salaam.
‘Dar es salaam tumepima madereva walevi X-Mass, tulikuta watu 135 wametumia kilevi na 34 walikuwa wamevuka kiwango, K’ndoni wameongoza, K’ndoni tulikuta 52 wametumia kilevi na 19 walikuwa wamevuka kiwango ambacho kinatakiwa kisheria’-Mpinga
Aidha takwimu hizo zimeeleza kuwa kila madereva 100 wilaya ya Kinondoni Dar es salaam, madereva 25 wanatumia kilevi zaidi ya kiwango kilichoruhusiwa kisheria, kingine alichozungumza kamanda Mpinga ni kuwa tangu sikukuu ianze mpaka leo, DSM hakuna tukio la ajali lililotokea. Bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Jeshi la Polisi lilivyotangaza magari mapya yatakayoruhusiwa kubeba abiria, Bonyeza play hapa chini kutazama