CEO wa Simba, Barbara Gonzalez leo ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC kuanzia January mwakani.
“Nimetoa notisi ya mwezi mmoja ili nishiriki kuhakikisha kipindi kizuri cha mpito (transition) na makabidhiano (handover) na Menejiment mpya”
“Ni jambo la fahari kwangu kwamba chini ya uongozi wangu, kwa kushirikiana na Rais wa Heshima wa Klabu, Mwenyekiti wa Klabu, Bodi ya Wakurugenzi, Wafanyakazi wenzangu, Wachezaji, benchi la ufundi, Wanachama, Washabiki, Wafadhili na Wadau wetu wengine, klabu ilipata mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, ikiwemo kutwaa mataji, kuvutia Wafadhili na kuanza kuheshimika kama mojawapo ya vilabu vikubwa vya soka Afrika.
“Nimechukua uamuzi huu kwa sababu kubwa mbili: mosi, kutoa nafasi kwa Bodi Mpya ya Wakurugenzi itakayochaguliwa kwenye uchaguzi ujao kupata fursa ya kuchagua Mtendaji Mkuu na Menejimenti mpya itakayoendana a dira yao, pili kujipa nafasi ya kutimiza ndoto na fursa nyingine kwingineko”
“Kipekee nawashukuru wote tuliosafiri pamoja katika ndoto ya kuifanya Simba SC iwe kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma, ni uamuzi mgumu sana kuacha kazi unayoipenda na uliyoifanya kwa moyo wote lakini ni ukweli pia kwamba mambo yote mazuri huwa na mwisho”