Polisi wa Los Angeles wamemkamata Mwanaume aliyekuwa akiishi uchi chini ya Nyumba ya Mwanamke mwenye umri wa miaka 93 ambapo Familia ya Mwanamke huyo mzee iliripoti kusikia kelele zisizo za kawaida kwa muda mrefu na walidhani kwamba Wanyama walikuwa wakitafuta hifadhi chini ya Nyumba kabla ya kutoa taarifa kwa Polisi.
Polisi walipofika waligundua kuwa Mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina la Isaac Betancourt mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikuwa anaishi kwenye sehemu ya chini ya nyumba (floorboard) sehemu yenye urefu wa futi mbili, Polisi walijaribu kutumia Mbwa na gesi mara kadhaa kumtoa lakini Mwanaume huyo alikataa kutoka hadi Polisi walipolazimika kutumia gesi ya machozi.
Ricardo Silva ambae ni mkwe wa mwanamke huyo alisema kuwa Familia yao ilikua ikisikia kelele kutoka chini ya nyumba yao kwa muda mrefu lakini hawakuwa na ufahamu kuwa Mwanaume huyo alikuwa amejificha chini ya Nyumba.
Aidha Silva alisema tukio hili ni la kushangaza ingawa sio geni, kwani Watu wengi wasiokuwa na makazi mara nyingi hutafuta hifadhi kwenye Nyumba za Watu wengine.
Hivi sasa Mwanaume huyo anashikiliwa na Polisi kutokana na uvamizi alioufanya huku pia Familia ya Nyumba hiyo ikisema itafanya ukarabati wa kuziba eneo hilo ili kuepusha changamoto kama hiyo kujirudua tena.