Serikali imeendelea na jitihada za kuhakikisha inapunguza idadi ya vifo vya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano hapa Nchini ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 zilizotolewa na Wizara ya Afya zinaonesha jumla ya watoto elfu kumi na nane wenye umri chini ya miaka mitano hupoteza maisha kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa malezi bora tangu kipindi cha ujazuzito.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi cha Wataalamu Afya Mkoa wa Tabora RC Mwanri ametumia jukwaa kutoa elimu ya kumlinda Mtoto.