Saa chache baada ya kuiwezesha Al Ahly kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Pyramids FC na kuiweka Al Ahly kileleni, club ya Al Ahly imetangaza kumuongezea mkataba Kocha wake Pitso Mosimane Raia wa Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka miwili.
Ushindi wa Al Ahly sasa unaiweka kileleni ikifikisha point 28 ilizovuna katika mechi 10, ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Pyramids FC waliopo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Misri wakiwa wamecheza game 11 na kuvuna point 26.
Pitso ambaye ameandika rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza mwenye asili ya Afrika kutokea nje ya Taifa la Misri kuaminiwa kuifundisha Al Ahly, hadi sasa ana rekodi ya kutwaa vikombe vitano na Al Ahly akiwa amedumu kwa miaka miwili.
Mataji aliyotwaa ni Club Bingwa Afrika 2, African Super Cup 2, Egypt Cup 1, akimaliza nafasi ya pili na tatu katika club Bingwa Dunia ndani ya misimu miwili, amecheza mechi 83, ameshinda 59, kupoteza 7 na droo mechi 17.