Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson anategemea kukubali ofa kutoka kwa klabu ya Al Ettifaq inayoshiriki Ligi ya Saudia.
Henderson anatarajiwa kufanya uamuzi hivi karibuni, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akizingatia ofa ya kubadilisha maisha yake ambayo ingeongeza mshahara wake wa Liverpool mara nne.
Steven Gerrard, mchezaji mwenza wa zamani wa Henderson wa Liverpool, aliteuliwa wiki iliyopita kama meneja mpya wa Al Ettifaq na amekuwa na jukumu muhimu katika kumtafuta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

Jordan Henderson amepewa ofa ya kitita cha pauni 700,000 kwa wiki ili kujiunga na Al-Ettifaq .
Nahodha wa Liverpool atafanya mazungumzo na Jurgen Klopp katika muda wa saa 24 zijazo ili kujua mustakabali wake uko Anfield lakini uwezekano wa kuungana na Steven Gerrard, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa meneja wa Al-Ettifaq.
Henderson bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake Anfield ambao unaaminika kuwa wa thamani ya pauni 190,000 kwa wiki lakini Al Ettifaq wamedhamiria sana kumsajili hivi kwamba watakuwa tayari kumuongezea mshahara wake zaidi ya mara nne.