Nyota wa Nigeria Rema anaendelea kuvunja rekodi, haswa kwa kuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kwenye tuzo za BRITs 2024.
Sasa albamu yake ya kwanza ya Rave & Roses, imepata vyeti rasmi vya Platinum nchini Ufaransa. Hii inafanya Rave & Roses kuwa albamu ya pili ya Afrobeats kuwahi kufikia hadhi ya Platinum katika taifa la Ulaya.
Iliyotolewa mwaka wa 2022, Rave & Roses ilipata sifa ya kimataifa haraka.
Albamu, muunganiko wa Afrobeats na ushawishi wa Afro-rave, dancehall, na nyimbo za Kiarabu, ilianzisha Rema kama mtangulizi katika upanuzi wa kimataifa wa aina hiyo ya muziki.
Imechochewa na nyimbo maarufu kama vile Calm Down ambazo zilifika nambari tatu kwenye Chati ya Singles ya Uingereza na baadaye kushika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 ya Marekani kwa remix iliyowashirikisha Selena Gomez, Rave & Roses ilikonga nyoyo za mashabiki duniani kote.