Leo July 18 2016 mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametambulisha mfumo mpya wa malipo ya afya kwa kutumia kadi katika hospitali na vituo vya afya vya serikali katika wilaya ya Kinondoni.
Kadi hiyo itakua inauzwa kwa sh 40,000 na itatumika kwa mwaka mzima kwa mtu mmoja, lengo la kuanzisha mfumo huu ni kudhibiti ufujaji wa fedha ambazo wafanyakazi ambao sio waadilifu walikuwa wanazifuja. Kadi hizo ambazo ziko chini ya manispaa na zinatarajiwa kuanza kutumika kuanzia July 25 2016.
>>>’Tunataka tutoke kwenye huu mfumo wa transaction, mfumo huu wa kulipia kwenye dirisha unapoteza muda mwingi sana lakini zaidi ya hapo unaruhusu mianya ya rushwa’:-Ally Hapi
ULIKOSA HII YA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUWEWEZA KUWEKA BETRI KWENYE MOYO WA MTOTO KWA MATRA YA KWANZA