Hekaheka ya May 23, 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM imetokea Dar es Salaam ambako mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi anadaiwa kumbaka mwanafunzi wake wa kike anayesoma darasa la Saba.
Tukio hilo limetokea baada ya mzazi wa mwanfunzi huyo kumkabidhi mwalimu huyo mtoto wake ili amfundishe masomo ya ziada ‘tuition’ ambapo inadaiwa kuwa walikuwa wanabaki na mwalimu darasani baada ya muda wa masomo.
Mwalimu huyo ambaye aliomba awe analipwa Tsh. 1,000 kwa siku ili amsaidie anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 13 tangu akiwa anasoma darasa la Sita kabla ya kuamua kumueleza ukweli dada yake.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story…
HEKA HEKA: Aliyedaiwa kujiita mchungaji ambaka mtoto wa miaka mitano Dodoma