Mwanasiasa mkongwe na Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Salim Turky, amefariki usiku wa kuamkia September 15 akiwa Hospitali ya Tasakhta Global Zanzibar baada ya kuugua ghafla.
Turky alizaliwa Februari 11, 1963, alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae tangu 2010, amefariki akiwa Mwenyekiti wa Kampuni za Turky zinazoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na Visiwa vya Comoro.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2017 Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, Turky alitafuta ndege iliyompeleka Lissu Nairobi na kuwa Mdhamani wa Deni la kukodi ndege iliyokuwa inamilikiwa na FlightLink.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Turky pia alijitokeza kutetea Ubunge katika Jimbo la Mpendae kwa tiketi ya CCM, alifahamika zaidi kwa jina la ‘Mr White’.