Watu watatu Wamiliki wa maduka ya dawa Mkoani Tabora wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora wakituhumiwa kusababisha kifo cha Mama Mjamzito Ester Chimika na Mtoto aliyekuwa tumboni kwa kujifanya wahudumu wa afya.
Watuhumiwa hao ambao ni Ezekiel Kazimoto Masanja, Victoria Boniface Makamba na Regina Frolence Balaye wamepandishwa kizimbani kusomewa makosa mawili yaliyotendeka Machi 15,2020.