JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata mkazi wa Dar es Salaam eneo la Kimara Temboni mtaa wa Amani, Selemani Haruna (24) kwa tuhuma za kumuua binti wa kazi za ndani na kisha kuficha stoo mwili wa marehemu.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema jijini Dar es Salaam na kumtaja binti aliyeuawa kuwa ni Editha Charles (22).
Amesema uchunguzi wa awali umeonesha tukio hilo lilitokea Julai 6, 2022 majira ya asubuhi ambapo mtuhumiwa alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa kuweka balbu na alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Sh milioni 1.8 na kutoweka.