Baada ya Ali Othman (25) Mkaazi wa Mchangani Zanzibar Kufanikiwa Kuiba Amplifaya ya Mskiti wa shekhe Ameir Tajo kwahani Zanzibar na kisha kuiyuza na video zake kusambaa mitandaoni akionekana kuvunja na kujitwisha kwenye kiroba amlifaya hiyo na kisha kutokomea nayo
Ayo tv imefika eneo la tukio na kuzungumza na mwanakamati wa Mskiti huo baada ya Kijana huyo kuhukumiwa kwa makosa aliyotatenda ambapo Mwanakamati huyo amesema kijana huyo kabla ya kupenyeza mikono kwa kutaka kuichota amplifaya hiyo iliofungiwa awali aliitaka kuiba feni na kisanduku cha sadaka ambavyo vilimshinda kutoa ndipo alipoamua kuiba amplifaya hiyo kwa kuibeba kichwani
” Mbele ya hakimu Rashid magendo imeelezwa na mwendesha mashtaka wa serikali Raghida Said kwamba mnamo tarehe 7.7.2024 saa 11 jioni huko kwaalinatu wilaya ya mjini alivunja na kuingia katika mskiti wa Ameir tajo na Kisha kuiba empirifaya yenye thamani ya shilling laki 5 mali ya mskiti huo jambo ambalo ni kosa kisheria ”
” Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 12.8.2024 na idadi ya mashahidi 5 na mahkama kuridhishwa na ushahidi huo na kumhuku kosa la kuvunja atumikie chuo cha mafunzo miaka miwili na kosa la kuiba atumikie miaka 3 na kua jumla ya miaka 5. Hata hivyo mahkama imeamuru hukumu hizo ziende sambamba na mtuhumiwa huyo atatumikia chuo cha mafunzo miaka 3 “