Mwanaume mmoja jijini Mumbai, India, amejikuta katika hali ya aibu baada ya kujikojolea wakati wa tamasha akilaumu Waandaaji kwa tamasha hilo kushindwa kuweka Vyoo vya kutosha kwa Wahudhuriaji.
Sheldon Aranjo, Mtaalamu wa Vyombo vya Habari ambaye pia anasumbukuwa na kisukari na matatizo ya kutoweza kuzuia mkojo alieleza kuwa kulikuwa na Vyoo vitatu pekee kwa zaidi ya Watu 1,000 walioshiriki tamasha hilo ambapo Aranjo alisema alilazimika kuacha foleni ya choo baada ya kushindwa kustahimili hali hiyo jambo lililomfanya kujikojolea.
Kupitia chapisho lake katika mtandao wa LinkedIn, Aranjo alitoa picha ya suruali yake na kuandika kwa hasira, “Nililipa kuja kujikojolea kwenye tamasha la Bryan Adams.” Kisha aliwakosoa vikali Waandaaji na kuwataka kuweka miundombinu bora kwa ajili ya ustawi wa Wahudhuriaji wa matukio makubwa.
Tukio hilo limeibua mjadala mkali mtandaoni, huku wengi wakilaumu Waandaaji kwa kutoweka huduma muhimu kama Vyoo vya kutosha huku wakisisitiza umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya Wahudhuriaji badala ya kuzingatia faida pekee.