Mwanamke mmoja wa Chicago anayeshutumiwa kwa kumrubuni binti mjamzito nyumbani kwake na kumtoa mtoto aliyeko tumboni mwake kwa kisu karibu miaka mitano iliyopita akiri kosa la mauaji Jumanne na kuhukumiwa kifungo cha miaka 50 jela.
Clarisa Figueroa, 51, akiwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu na amevalia vazi lla manjano linalong’aa, hakutoa taarifa lakini alijibu “Ndiyo” Jaji wa Kaunti ya Cook Peggy Chiampas alipomuuliza ikiwa anaelewa angehitaji kutumikia kifungo chote mapema,vyombo vya habari viliripoti.
Waendesha mashtaka wamesema Figueroa alimnyonga Marlen Ochoa-Lopez mwenye umri wa miaka 19 kwa waya mnamo Aprili 23, 2019, baada ya kumshawishi kijana huyo hadi nyumbani kwake kwa ahadi ya kumpa nguo za bure mtoto wake ambaye bado hajazaliwa kisha Figueroa alipiga simu 911, akisema mwanamke huyo alijifungua na mtoto alikuwa hapumui.
Ochoa-Lopez alikuwa na ujauzito wa miezi tisa. Mtoto alikufa karibu miezi miwili baadaye.