Dominique Pelicot, mume wa zamani wa mwathiriwa wa kesi ya ubakaji nchini Ufaransa Gisele Pelicot, alipatikana na hatia na mahakama siku ya Alhamisi ya kumtumia dawa za kulevya mara kwa mara na kumbaka kwa takriban muongo mmoja.
Mahakama pia ilimpata na hatia ya kuwaalika makumi ya watu wasiowafahamu kubaka mwili wa Bi Gisele ambao haukuwa na fahamu nyumbani mwao.
Jopo la majaji lilimhukumu Dominique Pelicot kifungo cha miaka 20 jela.
Kesi hiyo ya ubakaji imeushangaza ulimwengu na kumgeuza Gisele Pelicot kuwa ishara ya ujasiri na ustahimilivu
Kesi hiyo iliyochukua miezi mitatu ilionesha jinsi Pelicot alivyomlewesha Gisele na kisha kurekodi video za unyanyasaji huo huku akiwaita Wanaume kupitia mitandao ya mtandaoni ambapo wengi wa washtakiwa walidai kuwa walidhani walikuwa sehemu ya mchezo wa hiari lakini ushahidi wa video ulionesha kuwa Gisele hakuwa na fahamu wakati wa matukio hayo.
Mwendesha mashtaka ameomba Pelicot afungwe miaka 20 jela huku Washtakiwa wengine 49 wakikabiliwa na vifungo vya kati ya miaka 4 hadi 18, Gisele, ambaye sasa ana miaka 72 alionyesha ujasiri mkubwa kwa kufichua mateso aliyopitia na kudai haki Mahakamani.
Kesi hiyo imeibua mijadala mikubwa Nchini Ufaransa huku Waandamanaji wakitoa wito wa sheria kali zaidi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia pia Gisele alisisitiza kuwa hana cha kuonea aibu na kwamba unyanyasaji huo haukuwa kosa lake.
Hukumu ya mwisho dhidi ya Pelicot na Washtakiwa wengine inatarajiwa kutolewa hivi karibuni huku kesi hiyo ikihesabiwa kuwa hatua muhimu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.